stori za bongo

  • Home
  • MAPENZI
  • VICHEKESHO
  • PICHA AMAIZING
  • AFYA

Wednesday, November 18, 2015

JE WAJUA MADHARA YA VIATU VYENYE ......... KWA MWANAMKE?BOFYA HAPA KUDODOSWA MENGI

 Unknown     12:49 PM     habari, HIGH HEELS, VIATU, WANAWAKE     No comments   


Kulingana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke wa kawaida ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku vikimnyima raha ya kutembea kwa uhuru.
Visigino virefu huhamisha uzito wa mwili kutoka kwenye visigino vya miguu mpaka kwenye magoti, mapaja na kiuno, na nguvu kubwa inayotumika huishia katika viungio vya mifupa (balls and socket) na kusababisha viwe vinasuguana na kuleta maumivu.

Kwa kawaida, miguu ya binadamu, hasa visigino, vimeumbwa ili kuutegemeza uzito wa mwili juu ya ardhi. Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa mwili kubebwa na kisigino kirefu, hivyo uzito wa mwili kushindwa kusawazika.

Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito, kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino. Hii husababisha miguu, kiuno, na mgongo kuwa katika hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya kiafya, ikiwemo kuteguka na kuvunjika.

Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo kusababisha magoti na misuli ya mapaja (tendons) kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili balansi. Kwa kuwa misuli inakuwa inafanya kazi kubwa, uwezekano wa kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za baadae huwa mkubwa.

    
Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya tendon kuwa mifupi, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi yake. Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu (ankle) , magoti, na mifupa ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea (stretch and relax) na hivyo kusuguana wakati wa kutembea, hali ambayo kama haikudhibitiwa mapema, madhara yake huwa ni makubwa kwa siku za baadaye. 

 Hatua/Steps za kufuata:
  • Anza na viatu virefu kiasi inchi 2 - 3 na ukiweza kuvimudu unaenda ukiongeza urefu wake, usijaribu kutoka kutokuwahi kuvaa viatu virefu na kuanza na vile virefu labda vya inchi nne na zaidi ni hatari na hutaweza kumudu. Hii itasaidia kuizoesha miguu yako kupata nguvu ya kutembelea viatu virefu.
Begin with a shoe that has a broad, low heel (2-3 inches) and plenty of support over your foot and on the heel.

  • Ukiweza kumudu mfano wa viatu hapo juu anza na vile vyenye urefu kiasi / kitten heels ili uweze kuizoeza miguu yako kuwa na balance ya kutosha
>>HUYU NDIE MTOTO ALIE MEZA SIMU KISA MCHUMBA AAKE KUTAKA KUIKAGUA SIMU HIYO..BOFYA HAPA UJIONEE<<
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

  • HIZI NDIO VUNJA MBAVU ZETU KALI ZA LEO.
    Hi kulikua na baba alikua anaishi na biniti yake,sikumoja binti akaja na boyfriend wake usiku ,baba alipokua kwa chumba chake akasikia yu...
  • VUNJA MBAVU NA PICHA KALI ZA VICHEKESHO ZA LEO...
  • JE WAJUA SIRI YA MAKALIO KWA MWANAMKE?IJUE HAPA
    Mwanamke anayejiamini huonekana wa Tofauti katikati ya wanawake wengi...   Silaha pekee kubwa anayopaswa kuivaa mwanamke yoyote ni CON...
  • JE WAJUA NAMNA YAKUMRIDHISHWA MPENZI WAKO PINDI MKIWEPO KATIKA HALI YAKUFANYA TENDO LA NDOA..BOFYA HAPA KUPATA MAUJUZI
    Bila kukosea hakuna jinsia ambayo hainamapungufu yake katika swala zima la mapenzi,udhaifu huu au kasoro hizi mara nying huambatana na ...
  • THAMANI YA MAPENZI YAKO KWA MPENZI WAKO YAKISHUKA LAZIMA UTAAMBIWA MAENENO HAYA....YAJUE MAPEMA
    UNAWEZA  kuambiwa maneno mengi sana kutoka kwa mpenzi wako, mazuri na mabaya lakini yapo ambayo yanatoa taswira isiyo nzuri. Jambo la m...
  • JE WAMJUA MTU MWEMBAMBA KULIKO WOTE DUNIANI?..CHEKI PICHA ZAKE HAPA
  • JE WAJUA MADHARA YA VIATU VYENYE ......... KWA MWANAMKE?BOFYA HAPA KUDODOSWA MENGI
    Kulingana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke wa kawaida ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Visigino virefu hufanya ngu...
  • JE WAJUA TIBA YA KUSAGIKA NA KUOZA KWA MENO KWA WATOTO WADOGO?BOFYA HAPA KUJUZWA.
    Watafiti wengi wameshindwa kubainisha dhahiri nini usababisha mtu kutafuna au kuuma meno usiku ili inahusishwa sana na minyoo, maambukiz...
  • JE WAJUA NIGERIA NDO NCHI INAYOONGOZA KWA FASHION NZURI ZA NGUO NAKUONGEZA MVUTO KWA MVAAJI WAKIKE?CHEKI HAPA FASHION ADIMU
    PRESS HERE
  • 5 TIPS ON HOW TO TREAT A WOMAN ON A DATE
    Women are hard to impress! Yes truly women are very hard to impress and satisfy. It is really an achievement if a guy can get the comp...

Pages

  • Home

Copyright © stori za bongo | Powered by STORI ZA BONGO
Design by STORI ZA BONGO | Blogger Theme by STORI ZA BONGO | Distributed By STORI ZA BONGO