stori za bongo

  • Home
  • MAPENZI
  • VICHEKESHO
  • PICHA AMAIZING
  • AFYA

Tuesday, January 5, 2016

THAMANI YA MAPENZI YAKO KWA MPENZI WAKO YAKISHUKA LAZIMA UTAAMBIWA MAENENO HAYA....YAJUE MAPEMA

 Unknown     11:45 AM     mahaba, mapenzi, MTOSO     No comments   


UNAWEZA kuambiwa maneno mengi sana kutoka kwa mpenzi wako, mazuri na mabaya lakini yapo ambayo yanatoa taswira isiyo nzuri. Jambo la msingi ni kuwa makini kupambanua.
Pointi ya msingi hapa ni lugha zenye ishara mbaya kwa wapenzi. Umewahi kujiuliza kuhusu hili? Umewahi kutafakari juu ya kauli chafu anazotoa mpenzi wako dhidi yako?
Kauli za maudhi, kashfa na hata matusi wakati mwingine, wewe unazichukuliaje? Rafiki zangu, kauli ya mtu inaweza kukutoa gizani na kugundua ukweli uliopo ndani yake, lakini kama hutakuwa makini, unaweza kuchukulia kama utani na kuuacha ukweli uendelee, mwisho unakuja kushtuka, umeshaachwa!
Hapa nimekuandalia kauli zenye ishara mbaya ya penzi lako. Ukiona moja kati ya kauli zifuatazo, basi kuwa na mashaka, kisha fanyia kazi, utagundua ukweli.


AKIKUAMBIA HUVUTII!
Kati ya kauli mbaya zaidi katika uhusiano ni pale mpenzi wako atakapokuambia huna mvuto! Haijalishi amekuambia akiwa katika hali gani; utani au akimaanisha, lakini neno hilo si zuri kuambiwa na mpenzi wako.Kuambiwa huvutii, katika mapenzi ni tusi kubwa. Nini maana ya mvuto basi? Nani umvutie? Ni wapita njia? Ofisini? Sokoni? Ana maana gani hasa?
Siku zote mvuto ni kwa ajili ya mpenzi wako, ndiyo maana mkawa katika uhusiano, hii inamaanisha ulimvutia ndiyo sababu akakukubali. Kukuambia huvutii si utani, ni kweli haoni mvuto na inawezekana penzi limeshachuja.
Inawezekana akawa anafanya mzaha, kama ndivyo, atasoma ulivyopokea, akiona umekasirika atarekebisha usemi wake haraka, kama ni vinginevyo ataendelea kushikilia msimamo wake, hata kama ni kwa utani, lakini atakuwa anakufikishia ujumbe wako kwamba huna mvuto, kwa maneno mengine humvutii, humfai; kwa hiyo muachane. Kuna nini tena hapo? Akili kichwani mwako.
ETI HUPENDEZI!
Hii ni kauli nyingine mbaya. Unapoambiwa: “Hujapendeza kabisa, yaani huna uwezo wa kupangilia nguo, kila siku unachemsha!” Ujue kuna hatari hapo, angalia mara mbili uhusiano wenu.
Kuambiwa hujapendeza kunashusha thamani yako na kuonekana huna ujanja wa kufanya uchaguzi mzuri wa mavazi. Huenda ni kweli hujapendeza, lakini hilo si la kubeza.


Anatakiwa kukuambia kwa upole namna ambavyo unatakiwa kuvaa na kuonekana nadhifu. Kwa maneno mengine, kukuambia hujapendeza ni kama anakusuta, hakukubali na unamuaibisha!
Bado kuna mengi ya kujifunza zaidi lakini kutokana na ufinyu wa nafasi yangu, naomba niweke kituo kikubwa hapa, wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!


>>BOFYA HAPA KUJUA MBINU KABAMBE ZAKUMFANYA MWANAMKE AKUTAFUTE KWA GARAMA YOYOTE<<
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

  • HIZI NDIO VUNJA MBAVU ZETU KALI ZA LEO.
    Hi kulikua na baba alikua anaishi na biniti yake,sikumoja binti akaja na boyfriend wake usiku ,baba alipokua kwa chumba chake akasikia yu...
  • VUNJA MBAVU NA PICHA KALI ZA VICHEKESHO ZA LEO...
  • JE WAJUA SIRI YA MAKALIO KWA MWANAMKE?IJUE HAPA
    Mwanamke anayejiamini huonekana wa Tofauti katikati ya wanawake wengi...   Silaha pekee kubwa anayopaswa kuivaa mwanamke yoyote ni CON...
  • JE WAJUA NAMNA YAKUMRIDHISHWA MPENZI WAKO PINDI MKIWEPO KATIKA HALI YAKUFANYA TENDO LA NDOA..BOFYA HAPA KUPATA MAUJUZI
    Bila kukosea hakuna jinsia ambayo hainamapungufu yake katika swala zima la mapenzi,udhaifu huu au kasoro hizi mara nying huambatana na ...
  • THAMANI YA MAPENZI YAKO KWA MPENZI WAKO YAKISHUKA LAZIMA UTAAMBIWA MAENENO HAYA....YAJUE MAPEMA
    UNAWEZA  kuambiwa maneno mengi sana kutoka kwa mpenzi wako, mazuri na mabaya lakini yapo ambayo yanatoa taswira isiyo nzuri. Jambo la m...
  • JE WAMJUA MTU MWEMBAMBA KULIKO WOTE DUNIANI?..CHEKI PICHA ZAKE HAPA
  • JE WAJUA MADHARA YA VIATU VYENYE ......... KWA MWANAMKE?BOFYA HAPA KUDODOSWA MENGI
    Kulingana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke wa kawaida ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Visigino virefu hufanya ngu...
  • JE WAJUA TIBA YA KUSAGIKA NA KUOZA KWA MENO KWA WATOTO WADOGO?BOFYA HAPA KUJUZWA.
    Watafiti wengi wameshindwa kubainisha dhahiri nini usababisha mtu kutafuna au kuuma meno usiku ili inahusishwa sana na minyoo, maambukiz...
  • JE WAJUA NIGERIA NDO NCHI INAYOONGOZA KWA FASHION NZURI ZA NGUO NAKUONGEZA MVUTO KWA MVAAJI WAKIKE?CHEKI HAPA FASHION ADIMU
    PRESS HERE
  • 5 TIPS ON HOW TO TREAT A WOMAN ON A DATE
    Women are hard to impress! Yes truly women are very hard to impress and satisfy. It is really an achievement if a guy can get the comp...

Pages

  • Home

Copyright © stori za bongo | Powered by STORI ZA BONGO
Design by STORI ZA BONGO | Blogger Theme by STORI ZA BONGO | Distributed By STORI ZA BONGO